Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza
Photo Credit To getty
Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza

Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza

Ujerumani imesema kuchaguliwa kwa Boris Johnson kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ni msimamo wa nchi hiyo, kujitoa EU.

Akizungumza kupitia televisheni ya Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Frank_Walter Steinmeier amesema

uamuzi uliofanywa na Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Teresa May kumchagua Johnson ni kuonesha wazi msimamo wake wa kuiongoza nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo amesema anamatumaini kuwa waziri huyo mpya wa Mambo ya nje wa Uingereza atasaidia kudumisha uhusiano uliopo na Ulaya.

Boris Johnson ni mmoja ya mawaziri kadhaa wapya waliochaguliwa, ambao walikuwa wakiunga mkono nchi hiyo kujitoa Jumuia ya Ulaya.

Moja ya kazi zake za kwanza kuzifanya ni kutembelea ubalozi wa Ufaransa mjini London, kuadhimisha siku ya Bastille Day.

PERCEPTIONS

Post source : http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160714_steinmeier_britain_eu

Related posts