Museveni aketi barabarani kupokea simu
Photo Credit To Bw Museveni alipokea simu kando ya barabara wilaya ya Isingiro, karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania
Museveni aketi barabarani kupokea simu

Museveni aketi barabarani kupokea simu

Je ushawahi kupokea simu ya dharura? Je wewe hujitenga vipi na watu waliokaribu nawe ima ni mkeo ama hata wafanyakazi wenza ili upokee simu ya kibinafsi?

Na je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu za kale zisizo na touchscreen?

Haya basi, Hayo sio maswali ya kipima joto … la!

Museveni
Image captionMuseveni aliwapungia mkono wapita njia akiendelea na mawasiliano

Rais wa Uganda Bw Yoweri Kaguta Museveni alizua kioja katika kijiji cha Kyeirumba, wilaya ya Isingiro karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari ili apokee simu “ya dharura”. Picha za kisa hicho zilipakiwa kwenye mtandao wa Facebook na afisa wake wa habari Don Wanyama.

Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.

Museveni
Image captionWenyeji walifurahia kuwa na mgeni ambaye hawakumtarajia

Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkono wapita njia.

Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.

Museveni
Image captionWenyeji walikuwa na la kumweleza kiongozi huyo wa taifa

Ilikuwa ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi barabarani.

Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.

Simu
Image captionJe wewe umewahi kuchukua hatua gani ya kushangaza ili upokee simu ya kibinafsi?

Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi barabarani.

”Kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?”

”Ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.

”Ama ilikuwa ni #Besigyexit?”, wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.

PERCEPTIONS

Post source : http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160712_museveni_roadside_phonecall

Related posts